Idara ya Kilimo umwagiliaji na Ushirika ina jumla ya Wafanyakazi 65 wanaoongozwa na Mkuu wa Idara hiyo Bwana Thomas Masanja Shilabu.
Kazi/majukumu ya idara ya kila siku:
a)Kutoa elimu ya ugani kwa wakulima juu ya uzingatiaji wa Kanuni bora za Kilimo ili kuongeza tija ya uzalishaji.
b)Kuhimiza matumizi ya Zana bora za Kilimo katika kuongeza ufanisi wa kazi shambani.
c)Kusimamia Kilimo cha Umwagiliaji kwa lengo la kuwa na uhakika wa upatikanaji wa maji shambani.
d)Kusimamia upatikanani wa pembejeo za Kilimo na kuhimiza matumizi yake
e)Kutoa Elimu ya Hifadhi bora ya mazao ili kupunguza upotevu wa mavuno na uharibifu unaotokana na Hifadhi hafifu.
f)Kuwezesha uongezaji thamani ya mazao
g)Kuimarisha masoko ya mazao na miundo mbinu ya kusafirisha mazao
h)Kufikisha kwa wakulima teknolojia mpya za uzalishaji kutoka vituo vya utafiki.
i)Kuunganisha Sekta binafsi na Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali katika kutoa elimu ya Ugani.
j)Kuhimiza Kilimo cha mboga mboga na matumizi kwa afya/lishe na kipato
k)Kusimamia Utendaji kazi wa Vyama vya Ushirika.
l)Kuhimiza wakulima kuazisha na kuimarisha Vyama vya Akiba na Mikopo.
Malengo makuu ya baadaye ya idara katika kuboresha kazi zake:
a)Uendelezaji na uboreshaji wa miundombinu ya umwagiliaji wa kilimo cha mpunga
b)Uendelezaji na uboreshaji wa huduma za ugani kwa maafisakilimo
c)Uboreshaji wa maghala kwa ajili ya hifadhi ya nafaka na pamba
d)Uendelezaji wa Teknolojia za usindikaji na ufungashaji wa mazao ya mpunga na alizeti
e)Uendelezaji na uboreshaji wa matumizi ya zana bora za kilimo
f)Uboreshaji wa mbegu bora za mazao na huduma za ugani kilimo kwa wakulima
Eneo la wilaya
Wilaya ya Maswa ina ukubwa wa Ha. 339,800 na kati ya hizo Ha. 247,500 zinafaa kwa kilimo na kwa wastani hekta 192,375 hulimwa kwa mwaka.
Umwagiliaji
Eneo linalofaa kwa kilimo cha umwagiliaji ni hekta 52,375 na zinazomwagiliwa ni hekta 1,777 sawa na asilimia 3.4. Skimu zilizojengwa ni saba (7) nazo ni Bukangilija hekta 307, Bukigi hekta 319, Ijinga hekta 410, Ikungulyasubi hekta 271, Buyubi B (Ng’haya) hekta 200, Pandagi (Masela) hekta 200 na Kinamwigulu hekta 65, pia ipo skimu ya umwagiliaji kwa njia ya matone katika kijiji cha Ngongwa kwa ajili ya umwagiliaji wa zao la pamba hekta 5.
Nguvu kazi
Wilaya inakadiriwa kuwa na watu wapatao 344,125 kati yao watu wenye uwezo wa kufanyakazi ni 165,180 sawa na asilmia 48 ya wakazi wote wa wilaya ya Maswa.
Hali ya hewa
Wilaya ya Maswa ni moja ya Wilaya kame nchini, wastani wa mvua kwa mwaka ni kati ya mm 450 mpaka mm1000.Wastani wa joto ni 26oC.Mvua fupi huanza mwishoni mwa mwezi Oktoba na kuendelea hadi katikati ya mwezi Mei.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.