Halmashauri ya Wilaya ya Maswa ni miongoni mwa Halmashauri 6 zinazounda Mkoa wa Simiyu zikiwemo Halmashauri ya Itilima, Busega , Meatu, Halmashauri ya Mji wa Bariadi na Bariadi vijijini.Halmashauri ya Wilaya ya Maswa ilianzishwa mwaka 1926 toka Mkoa wa Shinyanga na kujitegemea kama Halmashauri.
Wilaya ya Maswa ni kati ya Wilaya 5 zinazounda Mkoa mpya wa Simiyu. Wilaya nyingine zinazounda Mkoa wa Simiyu ni Bariadi, Busega, Meatu na Itilima. Kwa upande wa Mashariki inapakana na Wilaya ya Meatu, Upande wa Kaskazini hadi Kaskazini Magharibi inapakana na Wilaya ya Itilima,Kusini hadi Kusini Magharibi inapakana na Wilaya ya Kishapu (Mkoa wa Shinyanga) na Upande wa Magharibi inapakana na Kwimba (Mkoa wa Mwanza).
Eneo la Wilaya ni kilometa za mraba 3,398 kati ya hizi 2,475 zinafaa kwa shughuli za kilimo na ufugaji, wakati kilometa za mraba 77 ni hifadhi ya misitu na kilometa za mraba 846 ni miinuko ya mawe, vilima na vichaka
Kiutawala, Wilaya ina tarafa 3, Kata 36 Mamlaka ya Mji 1 yenye vitongoji 40, pia kuna vijiji 120, na vitongoji 510.Halmashauri ina jumla ya idara 13 na vitengo 6.
i).Idara ya Utawala na Utumishi
ii).Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
iii).Fedha na Biashara
iv).Idara ya Afya
v).Idara ya usafi na Mazingira
vi).Idara ya Maji
vii).Idara ya Ujenzi na Zimamoto
viii).Idara ya Kilimo,umwagiliaji na Ushirika
ix).Mifugo na uvuvi
x).Idara ya Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii na vijana
xi).Idara ya Elimu ya Msingi
xii).Idara ya Elimu ya Sekondari
xiii).Idara ya Ardhi na Maliasili
Aidha kuna vitengo vya Sheria, Ukaguzi wa Ndani, Ugavi; Teknolojia ,habari, mawasiliano na uhusiano, ufugaji nyuki na Uchaguzi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ni Kiongozi Mkuu, Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ni Mtendaji Mkuu upande wa Serikali za Mitaa.
Wilaya inaongozwa na BARAZA LA MADIWANI lenye wajumbe 50 kati yao 2 ni wabunge wa kuchaguliwa kwa mchanganuo ufuatao:-
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.