• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Mrejesho |
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Fedha
      • Afya
      • Ardhi na Mali asili
      • Maji
      • Ujenzi
      • Kilimo
      • Mifugo
      • Maendeleo ya Jamii
      • Usafi na Mazingira
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mipango na Ufuatiliaji
    • Vitengo
      • Tehama
      • Sheria
      • Ukaguzi
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Viwanda
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Sheria ndogo
    • Fomu
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Video

Madiwani waipongeza Serikali kwa kutoa mabilioni Maswa

Posted on: May 12th, 2022

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu wameipongeza serikali kwa kutoa fedha za  kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya hiyo

Hayo yalibainishwa katika kikao Cha robo ya tatu ya mwaka kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Maswa leo tarehe 12 Mei 2022.

Katibu wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa ndg. Simon S. Berege amesema serikali imetoa shs bilioni 12,132,146,392.39 kwa ajili ya  miradi mbalimbali katika wilaya yote ya Maswa  fedha hizo zitaweza kukamilisha miradi yote ambayo haijakamilika.

Pia ndg Berege ametumia kikao hicho kwa kuwapongeza watumishi wote na waheshimiwa madiwani kwa kumaliza vizuri robo hiyo na kuwa nafasi ya 27 kitaifa, na kwenye mradi wa EP4R unaotekelezwa na Waingereza, Maswa imekuwa nafasi ya pili kitaifa kwa kufanya vizuri.

Akitoa salamu za serikali Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe. Aswege Kaminyoge amempongeza Mhe. Samia Suluhu Hassani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha kutoka serikali kuu kwa asilimia 100%, ili ziweze kutumika katika miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Halmashauri ya Maswa ikiwemo Afya, Maji, Barabara, Elimu na sekta nyingine

Pia Mhe Mkuu wa Wilaya amewashukuru waheshimiwa Madiwani, Mkurugenzi na wataalamu kwa usimamizi mzuri wa mapato  ya fedha zilizotengwa kwenye 40% inayotokana na mapato ya ndani ili iweze kupelekwa kwenye miradi kwa ajili ya kukamilisha na kuzinduliwa katika mwenge wa uhuru.  Pamoja na 10% ya fedha zinazokwenda kwa vijana na wanawake  zitolewe kwa 100% ili kukuza mapato ya vikundi.

Mkuu wa Wilaya amewasisitiza waheshimiwa Madiwani na watendaji kutoa elimu juu ya umuhimu wa sensa ya watu na makazi katika jamii kupitia vikao mbalimbali ambavyo vitafanyika katika maeneo yao na agenda kubwa katika vikao hivyo iwe ni zoezi la sensa litakalofanyika Augusti 23, 2022.

Katika hatua nyingine Mkurugenzi Mtendaji ambaye alikuwa Katibu wa kikao hicho amewaeleza wajumbe kuwa changamoto zilizojitokeza amezichukua na ataenda kuzifanyia kazi na wataalamu wake ili kuhakikisha mipango yote ya maendeleo inakamilika kwa ubora wa hali ya juu.

Matangazo

  • MATOKEO YA USAILI WA MCHUJO May 30, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI May 20, 2022
  • TANZGAZO LA NAFASI YA KAZI May 26, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI May 27, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Mkuu wa Mkoa aipongeza Maswa kwa kupata hati safi

    June 27, 2022
  • Mkuu wa Mkoa afanya ziara katika kiwanda Cha pamba wilayani Maswa

    June 09, 2022
  • Madiwani wa Manispaa ya Moshi wanufaika na mafunzo Maswa

    May 26, 2022
  • Mratibu wa Sensa Wilaya atoa mafunzo kwa Kamati za sensa

    May 16, 2022
  • Tazama zote

Video

Fursa za uwekezaji Mkoani Simiyu
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Taarifa ya Mapato na matumizi
  • Mfumo wa FFARS
  • Mfumo wa IMIS
  • Mfumo wa PlanRep
  • Government Web Framework
  • Mfumo wa PREM
  • Maswa DC Mail Domain
  • Hotuba ya Mh. Waziri Mkuu PLANREP/FFARS
  • Mfumo wa MVC-MIS

Viunganishi linganifu

  • Tovuti ya Mkoa wa Simiyu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • TAMISEMI
  • Sekretariet ya Ajira
  • Ikulu
  • Baraza la Mitihani Tanzani
  • Wizara ya Elimu Tanzania
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Mwonekano wa Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Maswa

    Sanduku la Posta: 170, MASWA

    simu ya Mkononi: +255 282 750 271

    Simu: +255 282 750 271

    Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.